AUDIO | WEUSI FEAT. KHADIJA KOPA "PENZI LA BANDO" | Download Mp3 AIR WEUSI
AUDIO | WEUSI FEAT. KHADIJA KOPA "PENZI LA BANDO" | Download Mp3
(Tanzania, Dar es salaam, Jumatano 17 Februari, 2020): Kundi maarufu la HipHop kutoka
Tanzania, WEUSI kuuanza mwaka 2021 wa Bongo Flava kivingine. Baada ya kuachia kazi
yao ya mwisho mwezi Disemba 2020, kundi hilo kurudi tena na ‘Penzi la Bando’.
Kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotoka leo WEUSI wameweka wazi kuwa wapo njiani
kuachia kazi yao mpya itakayomshirikisha malkia wa muziki wa Taarab nchini Khadija Kopa;
kazi inayotarajia kutoka siku ya Ijumaa 19 Februari 2021.
Kazi hiyo iliyotaarishwa na Producer S2Kizzy kutoka Tanzania inawakutanisha Weusi na
Khadija Kopa kwenye uwanja mmoja; Weusi wakidhirisha umahiri wao katika miondoko ya
HipHop na Bongo Fleva huku malkia Khadija Kopa kwenye miondoko ya Taarab
akiunogesha wimbo huo kwa vionjo na melodi za Baibuda kuongeza utashi wa wimbo na
kuweka ladha tofauti na ile iliyozoeleka katika nyimbo za Hip
‘Penzi la Bando’ ni miongoni mwa nyimbo mpya 14 zitakazopatikana kwenye Album mpya
ya WEUSI iliyopewa jina la “AIR WEUSI” project ambayo imekuwa ikiandaliwa kwa muda
usiopungua mwaka mmoja.
Akiongea kwa niaba ya kundi la WEUSI, G Nako alithibitisha taarifa hii akisema:
“Tuna furaha kubwa sana kwakuwa tunazidi kuimarika, kukua kimuziki, na kupata nafasi
ya kufanya muziki wa aina tofuati kama kundi. WEUSI kama kundi imetuchukua muda
mrefu kidogo kuja na a full project kwasababu ya kupishana kwa muda na kazi zetu
binafsi kama wasanii lakini pia kutambua deni tulilonalo kwa mashabiki zetu ambao
wamekuwa hawatusikii mara kwa mara lakini hawachoki kutusapoti kila tunapoachia
kazi. Tunajisikia faraja kubwa sana kuwaletea kazi yetu mpya na Khadija Kopa na album
yetu ya AIR WEUSI hivi karibuni kwani tunatambua sappoti tunayopata kupitia muziki
wetu kwa kipindi hiki chote. Tunamshukuru pia mama yetu Khadija Kopa kwa heshima
aliyotupa kwa yeye kuweka baraka zake katika wimbo huu wa “Penzi la Bando” sio
rahisi kuona wasanii wa HipHop wakishirikiana na wasanii wa Taarab lakini Mama
hakusita kutoa mchango wake na kwa hilo tunathamini na kushukuru sana.”
WEUSI wameweka wazi pia kuwa siku hiyo ya Ijumaa 19 Februari wataachia na video ya
Penzi la Bando lakini vilevile Album ya AIR WEUSI intarajia kutoka tarehe 12 March 2021
kupitia platforms zote za kusikiliza, kununua na kupakua muziki. Kwa taarifa zaidi kaa karibu
na mitandao ya kijamii ya WEUSI au fuatilia ukurasa wao binafsi wa Instagram:
@weusiofficial .
KWA TAARIFA ZAIDI / MAWASILIANO / INTERVIEWS:
Email: stargazemgnt@gmail.com / Mawasiliano: Gufi (+255) 762 755 755.



No comments